Search This Blog
Sunday, June 14, 2020
"Aliyekula mahari ya mtoto ataitapika" - ACP Shana
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Jonathan Shana, amesema kuwa Jeshi hilo halitokuwa na huruma kwa yeyote ambaye, atamuozesha mtoto wake kwa sababu ya tamaa za mali na yeyote ambaye tayari amekwishapokea mahari ama kula chakula kwenye sherehe ya kupokea mahari hatomuacha salama.
Hayo ameyabainisha wakati akitoa taarifa ya namna ambavyo, Jeshi hilo lilivyoweza kuzima tukio la kuozeshwa kwa mtoto wa miaka 12, lilitokea katika Kata ya Mussa wilayani Arumeru na kusema kuwa matukio ya namna hiyo yamekuwa yakiwahusisha Wazee wa Mila pamoja na viongozi wa Vijiji wenye tamaa ya mali.
"Sasa ninasema kwa dhati ya moyo wangu, kamwe hatutakuwa na huruma kwa yeyote atayemuozesha mtoto wake kwa sababu ya mali na kama kuna yeyote ambaye amekwishapokea mahari kwa mtoto wake, hakika nitampeleka jela na kama kuna yeyote alikula hela ya ushenga ataitapika na kwa wananchi wa kawaida ama ndugu alikula chakula kwenye sherehe hiyo kitamtokea puani" amesema Kamanda Shana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment