Search This Blog

Tuesday, May 19, 2020

Vikosi vya India vyamuua kiongozi wa waasi wa Kashmir


Kamanda wa kundi la waasi katika jimbo la Kashmir pamoja na msaidizi wake wameuawa katika tukio la ufyatulianaji risasi kati ya waasi na vikosi vya serikali ya India, hatua iliyochochea maandamano ya wanaotaka kujitenga na India pamoja na makabiliano na polisi.

Msemaji wa kundi la kijeshi Pankaj Singh amesema mapigano hayo yaliyodumu kwa masaa 12 yalianza baada ya polisi wa India pamoja na wanajeshi kuufunga mji wa Srinagar, kufuatia taarifa kwamba kuna wanamgambo waliojificha kwenye mji huo.

Jeshi la polisi lilithibitisha kuuawa kwa kamanda huyo wa kundi la Hizbul Mujahideen, ambalo ni kubwa kabisa katika jimbo la Kashmir Junaid Ashraf Sahrai pamoja na msaidizi wake.

 Junaid ni mtoto wa kiongozi wa ngazi za juu wa kundi la wanaotaka kujitenga Mohamed Ashraf Sehrai. Wanajeshi watatu na afisa polisi walijeruhiwa kwenye tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...