Search This Blog

Monday, May 25, 2020

Umoja wa Ulaya watazamia mkutano wa kwanza wa kilele wa ana kwa ana


Maafisa na wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesema viongozi wakuu wa kanda hiyo huenda wakawa na mkutano wa kilele wa ana kwa ana katika wiki zijazo, ili kujadiliana juu ya bajeti ya pamoja na mfumo wa ufufuaji uchumi ulioathiriwa na janga la virusi vya corona.

 Tangu kufungwa kwa shughuli za kila siku mwezi Machi, Umoja wa Ulaya umepambana kuendesha shughuli zake kupitia vikao vya njia ya vidio ili kuzuwia kuenea kwa virusi vya corona. 

Wapo wachache mjini Brussels, wanaoamini kwamba majadiliano makali ya bajeti yanaweza kuendeshwa kwa njia ya mtandao, lakini mwanadiplomasia wa juu amesema hakuwezi kuwa na makubaliano kuhusu bajeti na mfuko wa ufufuaji uchumi bila mkutano wa ana kwa ana. 

Halmashauri kuu ya umoja huo inatarajiwa kupendekeza siku ya Jumatano, bajeti yake ya euro trilioni moja pamoja na mfuko wa ufufuaji uchumi.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...