Search This Blog

Wednesday, May 6, 2020

Umoja wa Afrika kuichunguza dawa ya Madagascar



Umoja wa Afrika (AU) unafanya mazungumzo na Jamuhuri ya Madagascar, ili kupata data za kiufundi kuhusu usalama na ufanisi wa dawa ya mitishamba iliyotangazwa hivi karibuni ambayo ilidai inazuwia na kutibu Covi-19.

AU imesema kuwa Kamishna wa tume ya Umoja wa Afrika inayohusika na masuala ya kijamii Amira ElFadil alifanya mazungumzo na balozi wa Madagascar nchini Ethiopia Eric Randrianantoandro tarehe 30 April na wameafikiana kuwa nchi wanachama wataupatia maelezo muhimu Muungano wa Afrika kuhusu dawa za mitishamba.

Baada ya kupata maelezo Umoja wa huo kupitia kituo chake cha udhibiti wa magonjwa - (Africa CDC), kitatathimini data zilizokusanywa kuhusu usalama na ufanisi katika tiba hizo asili dhidi ya virusi vya corona.

Dawa hiyo inayohusishwa na mmea wa Kichina unaoitwa Artemisia (pakanga) - ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.

Africa CDC ni taasisi ya Umoja wa Afrika inayosaidia nchi wanachama katika juhudi zao za kuimarisha mifumo ya afya na kuboresha uchunguzi, kukabiliana na dharura za magonjwa, kuzuwia na kudhibiti magonjwa.

Hata hivyo AU imesema kuwa tathimini yake ya madawa ya mitishamba itazingatia maadili ya kiufundi ya kidunia katika kukusanya ushahidi muhimu wa kisayansi kuhusu ufanisi wa mitishamba.

Hatua hii ya Umoja wa Afrika inakuja baada ya rais wa Madagascar Andry Rajoelina kushiriki kikao cha AU cha wakuu wan chi ambapo aliwafahamisha wenzake kuhusu dawa ya miti shamba ya Madagascar anayoamini inazuwia na kutibu virusi vya corona.

Hatua hiyo inawadia wakati ambapo marais karibu wanne wa Afrika wamesema wanaagiza kiasi kikubwa cha dawa ya mitishamba iliyosemekana kupatikana huko Madagascar kuwa ina uwezo wa kutibu virusi vya corona.

Marais wa Tanzania, Jamuhuri ya Congo, Guinea Bissau na Equatorial Guinea wote wamemaua kutuma ndege nchini Madagascar kuchukua dawa hiyo ya mitishamba.

Dawa za mitishamba ambazo mara nyingi hupatikana katika eneo huchangia pakubwa katika suala la afya kote barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...