Search This Blog
Thursday, May 21, 2020
Trump na Nancy Pelosi washambuliana vikali kwa maneno
Kwa mara nyingine Rais Doanald Trump wa Marekani ameshambuliana vikali kwa maneno na Nancy Pelosi, Spika la Bunge la Wawakilishi la nchi hiyo.
Katika mahojiano na kanali ya televisheni ya MSNBC Pelosi amemlinganisha Trump na mtoto aliyevaa viatu vilivyotapakaa kinyesi cha mbwa. Akitoa radiamali kuhusiana na matamshi ya Trump spika huyo wa bunge la wawakilishi la Marekani amesema kuwa rais huyo wa Marekani ataendelea kuwa sawa na mtoto ambaye amevaa suruali iliyochafuka kwa na matope. Kabla ya hapo pia Nancy Pelosi alimkosoa Trump kutokana na maneno yake juu ya matumizi ya kidonge kimoja cha Hydroxychloroquine kila siku kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona na kusema kuwa, kutokana na rais huyo kuwa mwenye umri mkubwa na mnene wa kupindukia, hapaswi kutumia dawa hiyo.
Katika radiamali yake dhidi ya Pelosi, Trump amemtaja spika huyo wa bunge la wawakilishi kuwa ni mwanamke mgonjwa na mwenye matatizo mengi. Ushauri wa Trump wa kutumia dawa ya Hydroxychloroquine kwa mara nyingine umeibua ukosoaji mkali katika vyombo vya habari dhidi ya rais huyo. Ni miezi kadhaa sasa ambapo Trump na Pelosi wamekuwa wakishambuliana kwa maneno moja kwa moja, mashambulio ambayo yameongezeka ndani ya wiki hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment