Search This Blog

Tuesday, May 26, 2020

Serikali ya Ireland yaahidi kutoa euro milioni 5.5 Tanzania

Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Waziri wa maendeleo ya kimataifa na Diaspora wa Jamhuri ya Ireland Ciaran Cannon yaliyolenga kuangalia hatua ambazo nchi hizo zimechukua kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Serikali ya Ireland imeahidi kutoa fedha kiasi cha Uero milioni 5.5 ambazo zitatumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Benjamin Mkapa ambazo zitakwenda kulipa mishahara ya watumishi na kuajiri wafanyakazi wapya 169 kabla ya mwezi Desemba 31 ambao watatumika kuwafuatilia watu mbalimbali ambao wamekutwa na virusi vya corona.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...