Sanchi aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia mitandaoni, kwenye ukurasa wake wa Instagram, amewasisitiza mabinti kutumia kipindi hiki cha mfungo kuomba ili kupata mume mwema.
“Mabinti wenzangu katika imani siku zilizobaki kabla mwezi mtukufu hujaisha tusiache kumuomba Allah aliyetukuka atupe sote mume bora. Mume mwenye kheri na mcha Mungu, mume atakaekupenda na kukuheshimu na kuiongoza familia vizuri kwa ajili ya Allah,” ameandika Sanchi
Itakumbukwa, Aprili 24 mwaka huu, #Sanchi alislimu na kuwa Muislamu ambapo hivi sasa jina lake ni Surraiya.
No comments:
Post a Comment