Search This Blog

Thursday, May 21, 2020

RC Zambi amtaka DED wa halmashauri ya Kilwa awachukulie hatua kali watumishi wa kituo cha afya



Na Ahmad Mmow, Lindi.

Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kilwa, Renatus Mchau awachukulie hatua kali za kinidhamu baadhi ya watumishi wa kituo cha afya cha Pande ambao wamekopeshana fedha zilizokusanywa na kituo hicho.

Zambi alitoa agizo hilo katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kilwa baada ya kubaini watumishi hao wamekopeshana fedha zilizokusanywa na kituo hicho kwa ajili ya kununulia dawa na matumizi mengine ya kituo hicho.

Alisema nijambo lisilokubalika kuona fedha hizo zinatumika vibaya huku zikitakiwa kutumika kwa maslahi mapana ya umma.¥ Alisema tabia ya kutumia fedha vibaya inasababisha upungufu wa dawa kwenye vituo vya afya na zahanati.

Hivyo kusababisha wananchi kukosa huduma kwenye vituo hivyo vya kutolea huduma za afya.

Zambi alibainisha kwamba kituo hicho utendaji wake hauridhishi. Huku akiweka wazi kwamba asilimia 50 ya  fedha zinazokusanywa zinatakiwa kununulia dawa.

Hata hivyo baadhi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali hazitekelezi sharti hilo. Badala yake wanatumia chini ya asilimia 50 ya fedha zinazokusanywa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...