Search This Blog

Friday, May 15, 2020

PROF. MBARAWA AFANYA UTEUZI WA WAKURUGENZI MAMLAKA ZA MAJI



UTEUZI WA WAKURUGENZI WA MAMLAKA ZA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA – ARUSHA NA SUMBAWANGA

Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Arusha na Sumbawanga kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia leo tarehe 15 Mei, 2020.

Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imewataja walioteuliwa kuwa ni Mhandisi Justine Gordian Rujomba anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), na Mhandisi Gibon Nzowa anayekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Sumbawanga (SUWASA).

Uteuzi huo umefanyika chini ya Sheria Namba 5 ya Usambazaji Maji Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019. Aidha,  Wakurugenzi walioteuliwa watakuwa Makatibu wa Bodi za Wakurugenzi katika mamlaka hizo.


Kitengo cha Mawasiliano




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...