Search This Blog
Tuesday, May 5, 2020
Mwakyembe aunga mkono ligi irejee, atahadharisha TTF bila mashabiki wachezaji watakosa chakula
Waziri wa Michezo Dk Harrison Mwakyembe ameunga mkono suala la kurejea kwa ligi kuu lakini ametahadharisha kuwa unahitahijika mkakati madhubuti wa Serikali na TFF kuhakikisha hilo linafanikiwa vizuri.
Wakati huo huo Dk Mwakyembe amelitaka Shirikisho la Soka nchini TFF kufanya mawasiliano na FIFA kwa ajili ya msaada wa kifedha ili kuvinusuru vilabu vya soka kiuchumi kwani kucheza bila mashabiki hali itakuwa ni mbaya sana.
Hata hivyo leo hii (Mei 5, 2020) TFF ilitoa taarifa ya pamoja na TPLB wamesema kwamba wanaendelea na mchakato wa ndani kuelekea kurejea kwa ligi.
Hatahivyo taarifa hiyo imeongezea kwamba kurejea kwa ligi hiyo hatahivyo kutetegemea uamuzi wa serikali ambayo itatangaza muda mwafaka wa kurudi kwa ligi hiyo.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba kwa sasa mchakato huo ni wa ndani na kwamba wanachama wa shirikisho hilo wanapaswa kutekeleza agizo la awali la kuepuka mikusanyiko.
Wamesema kwamba watatoa muongozo mwengine baada ya kupata muongozo wa serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment