Search This Blog

Sunday, May 10, 2020

Mkuu wa zamani wa polisi ajiunga na kundi la Taliban


Mkuu wa zamani wa polisi amejiunga na kundi la Taliban katika mkoa wa Magharibi wa Farah, wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan imesema.

Taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa Meja jenerali Abdul Jalil Bakhtwar ambaye aliwahi kuwa mkuu wa polisi katika mkoa wa Farah kati ya mwaka 2002 hadi 2004, amejiunga na wanamgambo hao wanaoipinga serikali ya mjini Kabul.

Wizara hiyo imeonyesha kusikitishwa na hatua ya afisa huyo kujiunga na Taliban ikisema amejiunga na maadui wa watu wa Afghanistan.Kundi la Taliban limethibitisha kuwa Bakhtwar amejiunga nao pamoja na watu wengine na kuwa amekaribishwa vizuri.

Akizungumza na shirika la habari la DPA mwanawe Bakhtwar, Masoud Bakhtwar ambaye ni naibu gavana wa mkoa wa Farah amekanusha vikali kuwa babake amejiunga na Taliban.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...