Search This Blog
Sunday, May 10, 2020
Manchester united wachezaji waambiwa wajiandae kufua jezi
Taarifa zinaeleza kuwa Ligi Kuu ya England inaweza kurejea Juni 8 ambapo kutakuwa na maandalizi mafupi ya muda wa wiki tatu kwa timu shiriki na wachezaji pia watawekwa karantini kabla ya kuanza kucheza.
Nyota wa timu ya Manchester United wameambiwa kuwa wanatakiwa kuanza kujifulia nguo zao wenyewe kuelekea kurejea kwa mazoezi Mei 18.
United inajiaandaa kurejea kwenye mazoezi baada ya Ligi Kuu ya England kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Wachezaji wa United pia wanatakiwa kutumia usafiri binafsi wanapokwenda mazoezini Uwanja wa Carrington na wanatakiwa kuoga kwenye mabafu ya nyumbani kwao
Maamuzi ya kutakiwa kuosha na kufua vifaa vyao vya mazoezini ni kwa sababu hakutakuwa na huduma hiyo kwa kipindi cha hivi karibuni na wale wachezaji waliosafiri nje ya England kujitenga Sikh 14 pale watakaporejea ili kuona kama wana maambukizi ya Corona.
Manchester United ipo nafasi tano Kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 45 kibindoni baada ya kucheza mechi 29 na kinara ni Liverpool mwenye pointi 82 baada ya kucheza mechi 29.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment