Search This Blog
Sunday, May 24, 2020
Makonda Amtaka Mkandarasi Kukamilisha Barabara Ya Sinza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kwa mmoja wa wasimamizi wa barabara hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amemtaka Mkandarasi anayejenga Barabara ya Sinza inayoanzia Bamaga hadi Shekilango kuhakikisha Ujenzi unakamilika kwa Wakati ili kupunguza kilio cha foleni kwa watumiaji wa njia hiyo.
Makonda amesema barabara hiyo inayojengwa ina urefu wa Km 3.7 na upana wa Mita 22 ambapo itakuwa na Njia nne za Magari pamoja na Barabara ya watembea kwa miguu, Taa za Kisasa, Mitaro ya Maji na Bustani.
Aidha RC Makonda amesema ujenzi huo unaenda sambamba na ujenzi wa Barabara unganishi ikiwemo ya Kuelekea Kebbys hotel, Chuo cha ustawi wa jamii, Mwenge TRA, Sinza Mapambano, Lion hotel, Sinza meeda na Barabara ya Sinza Makaburini.
Pamoja na hayo RC Makonda amewaelekeza Viongozi wote wa Mkoa, Wilaya na Jiji kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi na kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliokusudiwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment