Search This Blog

Thursday, May 28, 2020

Mahadhi fiti kuibeba Yanga

By Oliver Albert na Thomas Ng'itu

WINGA Juma Mahadhi hatimaye amerudi rasmi  mazoezini  katika kikosi cha Yanga baaada ya kukaa nje ya uwanja kwa mwaka mmoja na miezi tisa kutokana na majeraha ya goti.
Mahadhi aliumia goti katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Yanga na USM Alger ya Algeria uliofanyika Agosti  19, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuumia , winga huyo alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Filbert Bayi Kibaha lakini baadae goti lilitunga tena usaha hivyo kufanyiwa upasuaji mwingine kwenye kitengo cha Mifupa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi).
Leo ikiwa imetimka mwaka na miezi tisa, mchezaji huyo amefanya mazoezi ya nguvu na wenzake na kuonyesha kuwa yuko fiti na wakati wowote anaweza kuunganishwa katika kikosi cha  wachezaji watakaocheza mechi zijazo zikiwemo za Ligi Kuu Bara.
Katika mazoezi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa  Chuo cha Sheria Ubungo, Mahadhi alionekana kwenda sawa katika kila mazoezi waliyokuwa wakipewa na kocha msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa.
Mkwasa aliwagawa wachezaji wake mazoezi ya kukimbia kwa kasi kutoka upande mmoja wa uwanja kwenda mwingine huku akiwahesabia namba na kisha kuwapangia machuma matano kuwataka kuyaruka  mazoezi ambayo Mahadhi aliyamudu.
Baadae Mkwasa aliwagawa wachezaji kwa timu mbili na kucheza Kama mechi,  na kisha kumuweka mahadhi nje ambapo aliendelea kupewa mazoezi binafsi .

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...