Search This Blog

Monday, May 18, 2020

Lijuakali amwaga chozi bungeni, aiomba CCM impokee

Mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Peter Lijualikali amelieleza Bunge kuwa uamuzi wa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe kuwa wabunge wote wa chama hicho wajiweke karantini kwa siku 14 hayakuwa makubaliano ya wabunge bali amri ya kiongozi huyo uamuzi ambao hakukubaliana nao tangu awali.

Akiwa analia kwa uchungu Lijuakali alisema "Mheshimiwa spika mimi niliingia bungeni lakini sijalala siku mbili kwasababu ya maumivu, mimi nimelala jera miezi sita kwasababu ya CHADEMA kwasababu ya chama changu leo natekeleza wajibu wangu naambiwa ni kwasababu ya posho  mh. spika nimeumiatunalilia katiba mpya ya nchi  wakati ya kwetu ya CHADEMA TUNAIVUNJA"

"Kiuhalisia uamuzi wa kuambiwa tusije bungeni haukuwa wa kidemokrasia wala hapakuwa na makubaliano yoyote palikuwa na amri. Watu wanaambiwa tumefuata posho wakati nimekuja kufanya kazi yangu ya kibunge. Mimi nimekaa jela miezi sita kwa sababu ya CHADEMA na imani yangu kwenye chama, leo nakuja kutimiza wajibu wangu naambiwa sababu ya posho"



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...