Search This Blog
Tuesday, May 5, 2020
Lema amjibu ndugai "Wabunge wa CHADEMA hawapelekeshwi"
Mbunge wa Arusha Mjini, kupitia CHADEMA, Godbless Lema, amesema kuwa kauli aliyoitoa Spika wa Bunge Job Ndugai, kwamba wabunge wa CHADEMA wanapelekeshwa, si ya kweli na aliitoa kwa dharula kwa kuwa chama chake kinaongozwa na watu wanaojielewa na hivyo hakuna mtu wa kumpelekesha mwenzake.
Mbunge Lema ameyabainisha hayo kauli ya Rais Magufuli ya kuzuia Wabunge wote ambao wamegoma kuhudhuria Bunge kutolipwa posho, ambapo Lema amesema uhai ni kila kitu na Corona imeua mwanafamilia wake hivyo hawezi kuleta mzaha.
"Kwanza siyo kweli, Wabunge wa CHADEMA hawapelekeshwi na mtu yeyote na ukitaka kujua sisi tuna Wabunge ndani ya chama wawili wametangaza kuhamia NCCR na hujasikia chama kimekaa, lakini maelekezo yalitolewa siku ambayo Waziri Mahiga alikuwa amefariki hivyo ilikuwa ni kauli ya dharula, na ndiyo maana Mwenyekiti amesema tunaendelea kuitafakari" amesema Mbunge Lema.
Aidha Lema ameongeza kuwa kulingana na hali ya maambukizi ilivyo kwa sasa, imefikia hatua hata yeye hachangamani na familia yake kwa kuwa amejitenga kwenye chumba chake pekee lengo likiwa ni kuiweka salama familia yake.
"Mimi hapa ninapoongea kwenye familia yetu tayari kuna mtu amekufa na ugonjwa huu, mimi hatari nimeiona kwa kina sana, mimi nimekuja nyumbani nimejitenga chumba na watoto wangu na siumwi na nina mtazama mke wangu kama Dada yangu".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment