Search This Blog

Thursday, May 7, 2020

Kijana Atumia Hela ya Kodi Kuchora Tatoo ya Wema. Sasa Hivi Familia yake inalala nje

Kijana Atumia Hela ya Kodi Kuchora Tatoo ya Wema. Sasa Hivi Familia yake inalala nje

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Papamafido ametumia kodi ya nyumba na kulazimika kulala nje baada ya pesa hiyo kwenda kuchorea ‘TATTOO’ ya Wema Sepetu.

Akizungumza na Bongo5, Papamafido amesema kuwa amelazimika kulala nje Miezi baada ya pesa za kodi kwenda kuchora ‘Tattoo’ ya Msanii wa filamu na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu huku kijana huyo akionyesha mapenzi yake kwa mwanadada huyo.

Papamafido ambaye hapo jana alibahatika kuonana uso kwa uso na Wema, alishindwa kuzuia hisia zake na kuvua shati lake alilovaa kisha kumuonyesha Wema Sepetu ‘Tattoo’ kubwa yenye sura yake aliyoichora nyuma ya mgongo na kumuacha Msanii huyo akishika mdomo pasipo kuamini mapenzi makubwa aliyoonyesha kijana huyo.

Mbali na kujichora huko ‘Tattoo’ iliyopelekea hadi baadhi ya ndugu zake kumtenga huku marafiki zake wa karibu kumcheka, lakini pia alikuwa na michoro mingine ambayo amemchora Wema Sepetu katika vibao na kumkabidhi

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...