Search This Blog
Tuesday, May 5, 2020
KENYA: Sababu za mji wa Mombasa kuathirika zaidi na corona
Huku janga la virusi vya corona likiendelea kusababisha madhara makubwa kote duniani mataifa ya Afrika mashariki hayajasazwa.
Licha ya viongozi wa mataifa hayo kusisitiza kuhusu umuhimu wa kufuata masharti ya shirika la Afya duniani kuhusu kukabiliana na virusi hivyo, ni asilimia ndogo ya raia wanaofuata maagizo hayo hatua inayoendelea kusababisha kuenea kwa maambukizi.
Nchini Kenya takriban wagonjwa 490 wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona wengi wao wakipatikana katika mji mkuu wa Nairobi na mji wa Mombasa.
Cha kushangaza ni kwamba maambukizi mapya yameripotiwa kwa wingi katika mji huo wa pwani ya Kenya ikilinganishwa na ule wa Nairobi ambao ndio mji mkuu wa Kenya.
Mji wa Mombasa kufikia sasa umeripoti zaidi ya wagonjwa 134 wa virusi hivyo, suala linaloendelea kuwatia hofu viongozi kutokana na kiwango cha maambukizi.
Kati ya visa 134 vilivyothibitishwa mjini humo, wagonjwa 36 wanatoka katika eneo bunge la Mvita na wengine 20 kutoka Old Town.
Hivyobasi wengi wamekuwa wakiuliza ni kwa nini Mji wa Mombasa umeathiriwa sana na Covid-19?
Mombasa ni mji wenye idadi kubwa ya Waislamu na tamaduni tofauti ukilinganisha na maeneo mengine ya taifa la Kenya.
Wakaazi wengi wa mji huo wamekuwa wakiishi kwa mshikamano mkubwa, wakishirikiana kwa karibu kwa kila jambo ikiwemo, kula pamoja, kufanya ibada kwa pamoja. Baadhi na hata huishi kwa pamoja kifamilia kama vile baba, mama na watoto kuishi na wajomba, bibi, wajukuu na kadhalika.
talii ndio uti wa mgongo wa mji wa Mombasa na eneo zima la pwani ya Kenya kwa jumla kutokana na hali yake ya hewa na mandhari mazuri ya kitalii ikiwemo fukwe za kuvutia za bahari.
Baadhi ya watalii wanaopendelea sana kuzuru mji huo wa pwani ya Kenya hutoka katika mataifa yalioathirika zaidi na ugonjwa wa corona kama vile Italia, Ujerumani na Marekani ambayo ndio kitovu kipya cha ugonjwa huo duniani.
Baadhi ya watalii hususan kutoka Italia wamepiga kambi na hata kuweka makao yao katika miji kama vile Malindi uliopo kaskazini kwa mji wa Mombasa.Madereva wa malori kutoka mataifa mengine ya Afrika mashariki wamekuwa wakizuru bandari ya Mombasa ili kubeba mizigo kupeleka katika mataifa hayo.
Raia wengi wamekaidi amri ya kujitokeza ili kupimwa kutokana na kuogopa gharama ya juu ya kukaa vituo vya karantini.
Mbali na kugharamikia malipo ya vituo hivyo waathiriwa pia wamesema kwamba vituo hivyo vina mazingira duni, hatua inayowafanya kuviona vituo hivyo kama maeneo ya kuwaadhibu na sio kuzuia maambukizi.
Hatua hiyo imerudisha nyuma vita dhidi ya ugonjwa huo kwa kuwa wengi wameamua kujificha licha ya kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment