Search This Blog
Wednesday, May 20, 2020
Iran yakosoa barua ya vitisho ya Trump kwa Shirika la Afya Duniani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema barua ya Rais Donald Trump wa Marekani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia haina umuhimu wowote na imeandikwa katika wakati usiofaa.
Sayyid Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyasema hayo katika ujumbe aliotuma jana Jumatano kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter na kufafanua kuwa, "ingawaje afya ya dunia ipo hatarini hivi sasa, na mataifa ya dunia yanahitaji ushirikiano na uongozi uliojikita katika sayansi wakati huu kuliko wakati wowote mwingine ule, lakini barua ya Rais wa Marekani imeingilia utendajikazi na uhuru wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO."
Katika barua hiyo ya vitisho kwa Tedros Adhanom Gabrayesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia na ambayo imekosolewa vikali katika kona mbalimbali za dunia, Trump alisema Marekani itaikatia misaada WHO kikamilifu iwapo haitapiga hatua kubwa za kujiboresha ndani ya siku 30 zijazo.
Kabla ya hapo, Dakta Kamal Kharrazi Mkuu wa Baraza la Kiistratijia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisisitiza udharura wa kukabiliana na uingiliaji wa kisiasa wa madola makubwa duniani katika asasi za kimataifa kama Shirika la Afya Duniani (WHO).
Alisema ili kudhibiti na kukabiliana na virusi vya corona, kuna haja ya kuwepo mshikamano na ushirikiano wa kimataifa chini ya mhimili wa WHO.
Wakati huohuo, Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetoa radiamali yake kwa barua hiyo ya Trump kwa mkuu wa Shirika la Afya Duniani na kusema kuwa, Rais huyo wa Marekani kwa kuzilaumu WHO na China kwa janga la corona, anakusudia kuficha uzembe wa serikali yake ulioifanya Marekani iwe muathirika mkubwa zaidi wa mlipuko wa corona duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment