Search This Blog

Tuesday, May 12, 2020

DRC yamuomba rais wa Zimbabwe apatanishe katika mgogoro wa mpaka na Zambia


Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC imemuomba Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe apatanishe katika mgogoro wa mpaka baina yake na Zambia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Bi Marie Tumba Nzeza, ambaye pia ni mjumbe maalumu wa rais wa nchi hiyo amekutana na Rais Mnangagwa katika ikulu mjini Harare na kumfahamisha kuhusu mgogoro huo.

Rais Mnangagwa ameombwa apatanishe katika mgogoro huo kama  mwenyekiti wa sasa wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Baada ya mkutano huo, Rais Mnangagwa amesema nchi hizo mbili zinataka SADC isuluhishe mgogoro huo.

Zambia na DRC zinahitilafiana kuhusu mpaka wao wa pamoja wenye urefu wa kilomita 1,600 ambapo mvuntano unahusu sehemu unakoishia mpaka huo.



Hii si mara ya kwanza kwa SADC kutakiwa kutatua mgogoro wa mpakani baina ya nchi wanachama. Katika muongo wa 90, SADC ilijaribu kupatanisha bila mafanikio mgogoro wa mpakani baina ya Botswana na Namibia kuhusu umiliki wa kisiwa katika Mto Chobe ambao uko katika mpaka wan chi hizo mbili.

Kesi hiyo hatimaye ilifikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ambayo mwaka 1999 ilisema kisiwa hicho ni milki ya Botswana.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...