Search This Blog

Saturday, May 9, 2020

Dk. Mwele Amemjibu Kigwangalla Atawashawishi Vipi Wakati Taarifa ya Hali ya Ugonjwa Hazitolewi?



Mkurugenzi wa kitengo cha kuzuia Magonjwa yasiyo ambukiza wa Shirika la Afya Dunia (WHO), Dk. Mwele Malecela amemjibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dk Hamis Kigwangalla, kuwa atawashawishi vipi watu waje wakati taarifa za hali ya ugonjwa hazitolewi.

“Kikubwa katika Pandemic hii ni pamoja na uoga. Utawashawishi vipi watu waje wakati taarifa za hali ya ugonjwa hazitolewe,” aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akimjibu Waziri Kigwangalla.

“Utajengaje imani? Kwa nini waache kwenda Mauritius na Namibia ambako hakuna cases?,” alihoji Malecela

Awali Kigwangalla amesema wameanza kujipanga ndani ya wizara ili kushawishi serikali yote kukubali namna ya kufungua biashara utali Juni 2020.

Amesema wamefanya utafutu kuna ajura 477,000 kupotea kutokana na hatua zinazochukuliwa na nchi mbalimbali.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...