
London,England. Wakati mkataba wake na Arsena ukibakiza mwaka mmoja, beki Mbrazil David Luiz (33) amefichua kuwa hana nia ya kustaafia soka klabuni hapo.
Badala yake Luiz amedai kuwa angependa amalizie soka la ushindani akiwa anachezea klabu yake ya moyoni Benfica ya Ureno ambayo ndio ilichangia kwa kiasi kumfanya awe staa mkubwa hivi sasa.
Beki huyo alisema kuwa hawezi kuficha mahaba aliyonayo kwa Benfica na anatamani kurejea tena kwenye klabu hiyo aliyoichezea kuanzia 2007 hadi 2011 baada ya kujiunga nayo akitokea Vitoria ya Brazil.
"Siku zote nimekuwa nikisema kuwa nitapenda kumalizia maisha yangu ya soka pale Benfica.
Katika mpira wa miguu kila kitu kinabadilika. Kilicho cha kweli leo kinakuwa cha uongo kesho lakini kwangu haiko hivyo.
Ninaipenda Benfica.Ndoto zangu ni kuwepo kiwanjani nikiwa na rangi zao. Kwa yote niliyoishi na kuwaza, kwa kile kilichoifanya Benfica kuwa maishani mwangu na kwenye historia yangu, kwa kila kitu, Benfica ni kubwa kuliko mchezaji yeyote," alisema Luiz.
Luiz ametoa kauli hiyo licha ya hamu ya kocha wa Arsenal Mikel Arteta kutamani kuendelea kubakia naye klabuni akikoshwa na sifa za uongozi alizonazo.
No comments:
Post a Comment