Search This Blog
Wednesday, May 6, 2020
Corona na ongezeko la wazee kufariki dunia mjini New York
Viongozi wa jimbo la New York nchini Marekani wameelezea kufariki dunia watu wengine 1,700 katika vituo vya kuwalea wazee ndani ya jimbo hilo kutokana na virusi vya Corona, idadi ambayo ilikuwa haijasajiliwa.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Andrew Cuomo, gavana wa New York, hadi sasa watu 4,813 wamefariki dunia katika vituo vya kulelewa watu wazima katika jimbo hilo kutokana na virusi hivyo hatari vya Corona. Kwa mujibu wa viongozi wa jimbo la New York wazee hao 1,700
waliofariki dunia katika vituo hivyo, hawakuwa wamesajiliwa. Inaelezwa kwamba, idadi kamili ya watu waliopoteza maisha katika vituo vya kulelea watu wazima ndani ya jimbo hilo kutokana na ugonjwa wa Covid-19 haijulikani. Jimbo la New York ndilo lenye idadi kubwa ya wahanga na waathirika wa virusi vya Corona kati ya majimbo yote ya Marekani. Hivi sasa vituo vya kulelea watu wazima na jela za Marekani ndiyo maeneo yaliyoathirika zaidi na virusi hivyo.
Wakati huo huo Rais Donald Trump wa Marekani amedai kuwa kuenea virusi vya Corona kwa Wamarekani, kunatoa fundisho kuwa yeye ndiye mwenye haki. Trump ambaye licha ya kukosolewa vikali kutokana na udhaifu wa utendajikazi wake mbovu katika kukabiliana na virusi vya Corona na pia kuwa ya juu idadi ya waathirika na wahanga nchini humo, amedai katika mahojiano na gazeti la New York Post kwamba, kuenea virusi hivyo angamizi kumewathibitishia watu wote kwamba yeye ndiye mwenye haki. Kadhalika ameonyesha matumaini kwamba Wamarekani wataweza kurudi katika hali yao ya kawaida hivi karibuni. Amezidi kufafanua kuwa, mgogoro wa kiuchumi unaotokana na virusi vya Corona na kupelekea watu milioni 30 kuomba bima ya kazi, utamalizika karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment