Search This Blog
Thursday, May 7, 2020
Aubameyang apewa makavu yake Arsenal
Kauli ya Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, kuhusu kwamba hawezi kumbembeleza mchezaji kusalia ndani ya klabu hiyo kama hana nia ya kuendelea kuwa hapo, moja kwa moja inaelezwa imemlenga staa wa timu hiyo, Pierre–Emerick Aubameyang.
Kwa siku za karibuni, Aubameyang ameonekana kugoma kusaini mkataba mpya ndani ya Arsenal wakati ule wa awali ukitarajiwa kumalizika Juni, mwakani.
Wakati Aubameyang akigoma kusaini mkataba huo, amekuwa akihusishwa kutakiwa na klabu kadhaa ikiwemo Barcelona, Real Madrid na Manchester United.
“Siwezi kumshawishi mchezaji kucheza Arsenal au kujiunga na sisi, mchezaji anatakiwa kujitoa na kupambana kwa ajili ya klabu,” alisema Arteta alipoulizwa mipango yake ya usajili na namna ya juhudi zake za kuwashawishi mastaa wasiondoke klabuni hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment