Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema nchi ambazo zinataka kuondoa marufuku zilizowekwa katika kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona zinapaswa kukidhi masharti yanayohitajika kuzuia maambukizi mengine.
Akizungumza leo na wanadiplomasia mjini Geneva, Ghebreyesus amesema hatua ya kulegeza njia za kijamii na kiuchumi lazima zifanyike kwa uangalifu sana.
Ameonya iwapo jambo hilo litafanyika kwa haraka, watakuwa wanaweka hatari ya kuibuka tena kwa maambukizi ambayo yanaweza kuwa mabaya zaidi kuliko hali iliyopo sasa.
Amesema serikali zinapaswa kuhakikisha kwamba maambukizi ya virusi ya corona yamedhibitiwa na mifumo ya afya ya kitaifa lazima iwe na uwezo wa kugundua, kupima, kuwatenga na kuwatibu wagonjwa wapya.
Pia Ghebreyesus amesema hatua za kuzuia maambukizi lazima ziwekwe kwenye sehemu za kazi, shuleni na maeneo mengine muhimu.

No comments:
Post a Comment