Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa lapongeza Uturuki kwa kutoa msaada katika jitihada za kkupamana na Covid-19.
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO laipongeza Uturuki kwa kutoa msaada katika mataifa tofauti katika juhudi za kupamabana na virusi vya corona.
Hans Kluge amesema kuwa nafahamu kile kinachofanya na Uturuki katika juhudi za kupambana na virusi vya corona.
Uturuki inatoa msaada wa vifaa vya matibabu na madawa kwa mataifa tofauti amesema Hans Kluge.
Kluge ameendelea kufahamisha kuwa msaada kutoka Uturuki kuelekea Uingereza, Italia, Uhispania na mataifa ya Balkans na jambo linalohitaji kupongezwa kwa kuwa malengo yake ni kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Mkurugenzi wa shirika la Afya la Umoja wa Mataifa katika eneo hilo amesema kwamba kitend hicho cha Uturuki ni cha kibinadamu.
Akijibu moja ya maswali kutoka kwa wanahabari, Kluge amesema kwamba Uturuki imetoa msaada wa vifaa vya matibabu na madawa kwa kiasi kikubwa kwa mataifa ya Ulaya kuliko mataifa mengine ulimwenguni.
Mkutano huo kati ya Kluge na wanahabari umefanyika kwa njia ya video, mkutano ambao suala zima kuhusu virusi vya corona na mbinu za kukabiliana navyo limejadiliwa.

No comments:
Post a Comment