Search This Blog
Tuesday, April 7, 2020
Waziri wa Afya Atumbuliwa KISA Kuipeleka Familia yake Baharini
Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern amemshusha cheo Waziri wa Afya, David Clark kwa kukiuka taratibu zilizowekwa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona nchini humo na kuipeleka familia yake baharini.
Waziri Ardern amesema katika mazingira ya kawaida angemfukuza kabisa kazi Clark kwa sababu kitendo alichofanya sio sawa na alitarajia atakuwa mfano kwa wengine.
Aliyekuwa Waziri wa Afya nchni humo Clark kwa sasa atakuwa katika nafasi za chini za baraza, Katika taarifa yake, amesema hakutumia busara na anaelewa kwa nini watu wamekasirishwa.
Hata hivyo New Zealand yenye watu Milioni 5 ilitangaza karantini ya nchi nzima mwishoni mwa mwezi uliopita na kufunga mipaka yake, shule, migahawa pamoja na sehemu nyingine zenye mikusanyiko ya watu.
Ikumbukwe kuwa Idadi ya maambukizi iliyoripotiwa nchini humo ni 1,160 na mpaka sasa kifo kimoja cha mgonjwa wa Corona kimerekodiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment