Search This Blog

Friday, April 10, 2020

Waamuzi wataja mambo matatu wanayoyakosa

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Wakati siku 30 alizotangaza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa za kusitishwa kwa shughuli za mikusanyiko ikiwamo za michezo zikielekea ukingoni, waamuzi wa soka nchini wameeleza mambo matatu wanayoyakosa.

Serikali ilichokua hatua hiyo ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona ambavyo vimeathiri dunia.

Mambo hayo ni pamoja na mazoezi ya pamoja waliyokuwa wakifanya, posho za kuchezesha mechi, kukutana na kushauriana katika mambo mbalimbali yanayohusiana na kazi yao.

Wakati waamuzi wakizungumzia corona kusimamisha ligi na hivyo kuwanyima fursa ya kuchezesha mechi, ligi ilipaswa kusimama kuanzia Machi 16 kupishia michuano ya kimataifa ya Afrika kwa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, ambapo Stars pia ilipaswa kushiriki michuano ya wachezaji wa ndani (Chan) huko Yaounde, Cameroun iliyokuwa imepangwa kuanzia kuanza Aprili 4 – 25.

Hata hivyo, waamuzi hao wamesema hawajayumba kiuchumi kwa kutochezesha mechi kwani mfumo wa kazi yao unawapa fursa ya kufanya majukumu mengine ya kuwaingizia kipato.

Wakizungumza na Mwananchi jana, baadhi ya waamuzi walisema kutofanya mazoezi ya pamoja imekuwa changamoto kwao kipindi hiki.

Advertisement

Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania, Hery Sasii alisema kuna tofauti ya kufanya mazoezi pamoja na utaratibu wa sasa wa mazoezi binafsi.

“Mnapokuwa pamoja kuna vitu vipya utajifunza, tofauti na unapokuwa peke yako, corona ni janga la dunia hivyo hatuna namna,” alisema.

Kuhusu kukosa kipato, Sasii alisema sio changamoto kubwa kwani mbali na kazi ya uamuzi, lakini utaratibu wao kila mmoja ana kazi nyingine inayomuingizia kipato nje ya uamuzi.

Mwamuzi mwingine, Frank Komba alisema licha ya corona kufuta utamaduni wao wa mazoezi, lakini pia kipindi hiki wamekosa kuingiza Sh350,000 ambazo ni ujira wa kuchezesha mechi moja ya Ligi Kuu.

“Malipo ya mechi moja ni Sh200,000 na per diem (posho ya siku) ambayo si chini ya 150,000, hivyo kuna pesa tumeikosa kipindi hiki, achilia mbali kutochezesha mechi kwa muda mrefu nako kunasababisha ile fitiness na ubora wa uelewa wa sheria kupungua,” alisema.

Alisema changamoto nyingine ni kushindwa kujadiliana laivu mechi walizochezesha kama ambavyo ulikuwa utaratibu wao wa awali.

Mwamuzi wa kike, Frolentina Zabron alisema janga la corona limewaathiri kwa kuondoa umoja wao wa miaka yote.

Alisema ili mwamuzi akae sawa katika kipindi hiki ni lazima ajisimamia, vinginevyo katika nidhamu ya mazoezi vinginevyo atakwama.

Makamu Mwenyekiti wa kamati waamuzi, Israel Nkongo alisema wamewapa maelekezo ya kufanya mazoezi binafsi nyumbani na mengine katika eneo lenye uwazi nje ya nyumba zao lakini kwa tahadhari.

“Kila mkoa una group la Whatsap ambako waamuzi wa mkoa husika wanatuma mle kila kinachofanyika kwenye mazoezi yao na baadaye clip zinatumwa kwetu. Zinapotumwa tunafuatilia mojamoja na kutoa maelekezo ya nini waboreshe, zoezi ambalo linafanyika kila siku,” alisema.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...