Search This Blog

Wednesday, April 8, 2020

Van Dijk: Aubameyang na Lacazette ni bonge la fowadi England

LIVERPOOL, ENGLAND . BEKI kisiki wa Liverpool, Virgil van Dijk naamini safu ya ushambuliaji ya Arsenal inayoundwa na wakali Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette ni bab kubwa kwenye Ligi Kuu England.
Beki huyo Mdachi alisema hilo wakati alipotaja kikosi chake cha wachezaji watano wanaokipiga kwenye Ligi Kuu England, akimchagua Aubameyang kuwa kwenye safu ya ushambuliaji. Van Dijk hakumchagua mchezaji yeyote anayecheza naye kwenye kikosi cha Liverpool.
"Kwa kil walichokifanya kwa msimu wote. Lacazette na Aubameyang ni washambuliaji matata," alisema.
"Ningeweza kumchagua pia Aguero, ni mshambuliaji mzuri na takwimu zake hazidanganyi tangu alipotua kwenye Ligi Kuu England."
Lakini, Van Dijk anaamini Aubameyang na Lacazette ndio washambuliaji moto kwenye ligi. Beki huyo amekabiliana na wakali hao wa Arsenal mara kadhaa na kusema anafurahishwa sana na ushirikiano wao ndani ya uwanja.
Aubameyang amecheza mechi 32 za michuano yote akiwa na Arsenal msimu huu na kufunga mabao 20. Kabla ya ligi kusimama kutokana na virusi vya corona, Auba alionyesha kiwango bora akifunga mabao manne katika mechi tano za mwisho. Kwa msimu huu, Aubameyang na Lacazette kwa pamoja wamefunga mabao 29.
Lacazette, yeye amecheza mechi 26 za michuano yote msimu huu na kufunga mabao tisa.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...