Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imeelezea wasiwasi kuhusu uchaguzi ujao nchini Poland, ikihofia kwamba kura hiyo inaweza isikidhi vigezo vya kimataifa.
Kamishna wa sheria wa Umoja wa Ulaya Didier Reynerds amesema leo kuwa ikiwa uchaguzi wa rais nchini Poland utaendelea chini ya mazingira ya sasa, unaweza kushindwa kufikia vigezo kadhaa vya kimataifa.
Amesema hayo wakati wa kikao cha kamati ya bunge la Ulaya, akinukuu taarifa kutoka shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE.
Uchaguzi wa rais nchini Poland umepangwa kufanyika Mei 10. Chama tawala cha Sheria na Haki kinataka uchaguzi huo ufanyike kote nchini kwa njia ya posta kutokana na janga la corona, lakini upinzani unataka uahirishwe.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment