Search This Blog

Thursday, April 2, 2020

TUJIKUMBUSHE : Bocco aizamisha Njombe Mji

By Mwandishi wetu


TAREHE kama ya leo miaka miwili tu iliyopita, wakati Simba ikijiandaa kunyakua taji lake la 19 la Ligi Kuu Bara, waliinyosha Njombe Mji na kuchangia kuishusha daraja msimu huo wa 2017-2018.

Ndio, Simba wakiwa chini ya Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre walifunga safari mpaka Njombe kuvaana na wenyeji wao kwenye Uwanja wa Sabasaba, mjini humo na Wekundu wa Msimbazi walitakata kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Utamu wa ushindi huo ulitokana na mabao yote mawili kuwekwa kimiani na nahodha wa Simba aliyekuwa akiichezea timu hiyo kwa msimu wake wa kwanza tangu aliposajiliwa kutoka Azam FC.

Bocco ambaye msimu huo alimaliza akiwa mabao 14 sawa na Marcel Kaheza ambaye kwa sasa yupo Polisi Tanzania, walishika nafasi ya pili katika orodha ya Wafungaji Bora nyuma ya kinara, Emmanuel Okwi aliyekuwa pia Simba aliyemaliza na 20, alifunga mabao hayo katika kila kipindi.

Bocco, alifunga bao la kwanza dakika ya 17, kisha kuja kuongeza la pili dakika ya 64 na kuifanya Wekundu hao kukaa kileleni na kwenda kubeba taji kwa mara ya kwanza baada ya kulisotea kwa misimu sita mfululizo tangu walipolitwaa mara ya mwisho mwaka 2012.

Simba ilimaliza msimu huo ikiwa na alama 69 baada ya mechi 30 na kufunga mabao 62, wakifuatiwa na Azam iliyokuwa na alama 58 na waliokuwa watetezi, Yanga walimaliza kwenye nafasi ya tatu na pointi zao 52.

Advertisement

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...