Serikali ya Syria imelaani ripoti ya Shirika la Kuzuia matumizi ya Silaha za Sumu - OPCW ambayo ilisema uongozi wa jeshi la Rais wa Syria Bashar al-Assad huenda ulitumia silaha za sumu katika eneo lililodhibitiwa na waasi mwaka wa 2017.
Televisheni ya taifa ya SANA, ikiinukuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni imesema serikali ya Syria inalaani vikali ripoti hiyo na kupinga kilichoandikwa ndani.
Taarifa hiyo imekanusha kuwa wanajeshi wa serikali walitumia gesi za sumu katika kijiji cha Latamneh na kwingineko nchini Syria.
Ripoti iliyotolewa jana ya wapelelezi walioteuliwa na OPCW iliyalenga matukio ya mji ambao wakati huo ulikuwa mikononi mwa waasi wa Latamneh mnamo Machi 24, 25 na 30 2017.
Ilisema kuna ushahidi wa kutosha kuamini kuwa jeshi la angani la Syria lilitumia gesi za sarin na kloroni kama silaha ya sumu.

No comments:
Post a Comment