Search This Blog

Tuesday, April 28, 2020

Shambulizi la kigaidi Afrin nchini Syria

Idadi ya watu waliofariki  kutokana  na shambulizi la kigaidi Afrin nchini Syria yafikia watu  40.

Watu 40 waripotiwa kufariki katika shambulizi la kigaidi lililoendesha na wanamgambo wa kundi la PKK/YPG  Afrin nchini Syria.

Miongoni mwa watu hao waliofariki wamo watoto  11.

Wizara ya ulinzi imefahamisğha kwamba  shambulizi hilo la magaidi limelenga eneo la Racu katika kitongoji cha Afrin nchini Syria na kusababisha maafa hayo.

Magadi wametumia bomu la kutengeneza kwa mikono na kuchanganya na mafuta.

Kama ilivyo kawaida yao  magaidi wa kundi la PKK na washirika wake wa YPG wamewalenga raia na kuwasababishia maafa.
Katika shambulizi hilo watu  47 wamejeruhiwa  wakiwemo pia watu waliojeruhiwa vikali.
 


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...