Search This Blog

Tuesday, April 21, 2020

Rais wa Sierra Leone ajiweka Karantini, mlinzi wake aambukizwa Corona


Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio amejiweka Karantini kwa siku 14 baada ya mlinzi wake kubainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corrna.

Msemaji wa ofisi ya rais amewaambiwa waandishi wa habari kuwa rais wao ana afya njema lakini atakuwa akifanya kazi zake akiwa nyumbani na hakuna mwanafamilia yake aliye athirika na virusi hivyo hadi sasa.

Katika ukurasa wake wa Twitter rais Bio ameandika ” Serikali yangu itaendelea kuwa na uwazi kwa wananchi ambao wanatakiwa kuendelea kujikinga kwa kufuata maelekezo yote”

Nchi ya Sierra Leone hadi kufika siku ya leo ina visa vya wagonjwa 43 wa covid 19, sita wamepona na hainavifo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...