Search This Blog
Wednesday, April 8, 2020
Mwizi wa "mask" ahukumiwa kifungo nchini Uingereza
Mtu ambaye aliiba mask ya upasuaji kutoka hospitali London, mji mkuu wa Uingereza, amehukumiwa kifungo cha miezi 3 jela.
Kulingana na polisi wa London, L.H mwenye umri wa miaka 34 aliiba barakoa 3 za upasuaji katika Hospitali ya Chuo cha King's London mnamo Jumapili.
Mtu huyo alikamatwa na maafisa usalama baada ya kushtakiwa na wafanyikazi walioshuhudia tukio hilo.
Mshutumiwa alifikishwa kortini Jumanne. Alikubali uhalifu wake mahakamani, na kuhukumiwa kifungo cha miezi 3.
Wataalamu wa huduma za afya wanasema wana uhaba wa vifaa vya kinga kupambana na maambukizi ya Corona(KOvid-19) nchini Uingereza.
Wiki iliyopita,daktari mmoja aliwaomba wagonjwa wake msaada wa vifaa vya kujikinga katika taarifa yake kwenye kituo cha Sky News .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment