Search This Blog
Wednesday, April 8, 2020
Mechi za Serie A zilizobakia kumalizwa bila mashabiki
UONGOZI Serie A nchini Italia unafikiria uwezekano wa kumalizia mechi zote 12 za ligi hiyo zilizosalia katika Jiji la Roma kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa COVID19.
Kwa mujibu wa gazeti la La Repubblica, chama cha soka nchini Italia, kinatafakari kwa kina namna ya kumalizia msimu huu, huku wakipata wazo hilo la kucheza michezo sehemu moja, jambo ambalo halijawahi kufanyika.
Kama ilivyo kwa Ligi zote na mashindano mbalimbali duniani, Serie ilisitishwa katikati ya mwezi uliopita kutokana na mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona.
Serie A inafikiria kumalizia mechi zote 12 za ligi hiyo zilizosalia katika Jiji la Roma kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona PICHA ZAIDI SOMA HAPA
Klabu zote 20 za Serie A zitakwenda Rome kumalizia msimu huu kwa muda wa siku 45, yaani mwezi mmoja na nusu kwenye mechi ambazo mashabiki hawataruhusiwa kuingia uwanjani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment