Search This Blog

Thursday, April 16, 2020

Manara wa Simba Aibua Upya hoja ya Mbunge wa CCM dhidi ya Yanga Kufananishwa na Kaya Maskini



Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara ameibua upya hoja ya Mbunge wa CCM jimbo la Nkasi Ally Kessy ambaye alitaka klabu ya Yanga iingizwe katika mpango wa kusaidia kaya masikini unaoendeshwa na mfuko wa maendeleo ya jamii (Tasaf).

Kessy aliwahi kutoa hoja hiyo kama masihara kwa waziri wa utumishi wa utawala bora George Mkuchika ambaye ni kada wa Yanga.

Msemaji huyo wa Simba ambaao ni watani wa jadi wa Yanga kupitia ukurasa wake wa instagram aliposti kipande cha video hiyo ya Kessy na kusema “Hili jambo ni muhimu sana, Lazma tutokomeze Kaya maskini sana na zisizojiweza. Huyu Mbunge Kessi ana akili sana na mawazo yake yafanyiwe kazi na Serikali fasta”

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...