
London, England. Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson huenda akakosa mechi zote za Ligi Kuu England zilizobaki msimu huu.
Hodgson (72) amepanga kutojitokeza katika mechi kwa kuhofia maambukizi ya virusi vya covid-19.
Kocha huyo wa zamani wa England, amewaambia marafiki zake hatakaa kwenye benchi au kuongoza mazoezi.
Hodgson anahofia kupata maambukizi hayo endapo atajitokeza katika mkusanyiko.
Timu zimepanga kurejea uwanjani kuendelea na ligi katikati ya mwezi Juni na huenda mechi hizo zikachezwa mbele ya mashabiki wasiozidi 300.
Hodgson amekuwa katika uangalizi maalumu katika kipindi chote tangu janga hilo lilipoibuka.
No comments:
Post a Comment