Search This Blog

Friday, April 10, 2020

Klopp afichua kisa cha kumpiga chini Mane

LIVERPOOL, ENGLAND . KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amekiri kwamba mara ya kwanza alipomwona staa wa timu hiyo, Sadio Mane mwonekano wake, akamwona hamna kitu.
Kocha huyo Mjerumani, ambaye alikuwa akiinoa Borussia Dortmund wakati huo, alitaka kumsajili staa huyo Msenegali, Mane alipokuwa akikipiga RB Salzburg.
Alifuta mpango huo wa kumsajili Mane baada ya kukutana naye na matokeo yake, akatimkia zake Southampton, ambako ndiko Liverpool walikomsajili kwa ada ya Pauni 34 milioni mwaka 2016.
Klopp alisema: “Nakumbuka mara ya kwanza kukutana na Sadio nilikuwa Dortmund. Alikuwa kijana mdogo, alivaa kapero. Alikuwa akionekana kama rapa hivi. Nikaona sija haja ya kumchukua, kipindi hicho timu yetu haikuwa mbaya kabisa.
“Mimi nilihitaji mtu wa kuja kuanza kumwendeleza tena. Nilikuwa na hisia hiyo juu ya Mane, lakini kumbe nilifanya kosa. Aliendelea zake kufanya vizuri Salzburg na alipoenda Southampton akaenda kuonyesha kabisa ubora wake.”
Mane amefunga mabao 77 katika mechi 181 alizochezea Liverpool chini ya kocha Klopp. Anatajwa kuwa kinara kwenye mbio za mchezaji bora kwenye Ligi Kuu England, akiwa amefunga mabao 14 msimu huu na kuisogeza kabisa Liverpool kwenye kubeba taji lao la kwanza lwa Ligi Kuu England, wakihitaji ushindi kwenye mechi mbili tu zijazo kujibebea taji.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...