Search This Blog

Sunday, April 12, 2020

Jere100 bado hajaisahau BSS

By Clezencia Tryphone

WASANII nchini wametakiwa kutambua mwanga walioupata kutokana na Shindano la BSS kwa kuwa ni moja ya njia yao ya mafanikio ya walipofikia hivi sasa.
Hivi karibuni imetokea sintofahamu kutoka kwa washiriki mbalimbali ya shindano hilo kulalamikia zawadi zitolewazo na wahusika wa shindano hilo wakidai haziwafii kama inavyotangazwa.
Akizungumzia hilo mshiriki wa BSS aliyeshika nafasi ya nne Kala Jeremiah amewataka wasanii wenzake na wajao watambue shindano hilo ni moja ya muongozo wa mwanga kwa msanii husika.
Amesema, kilichotokea hivi sasa ni moja ya changamoto hivyo sio kumtupia lawama mwanzilishi wa shindano hilo Madame Ritha kwani licha ya kuteleza ila awewafanya watu wengi watoke na kujilikana akiwemo yeye,
“Nimepigiwa simu sana na wanahabari, kuhusu zawadi za mshindi wa mwaka jana, mimi niseme ukweli kwamba, BSS imetupa mwanga sana wasanii sisi nikiwemo mimi, mwanga wa maisha ya usanii nimeipatia pale,” amesema.
Kala amesema, sio sahihi kuulaumu uongozi wa BSS kwa kosa moja lililojitokeza  bali wanatakiwa kusogelewa kwa ukaribu ili kufahamu tatizo ni lipi lilopelekea sintofahamu hiyo kwa sasa ili kuwapa moyo kutokana na ukombozi mkubwa walioufanya kuwainua wengi.
Hivi karibuni serikali iliitaka BSS kumlipa zawadi mshindi wa shindano la mwaka jana, Meshack Fukuta.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...