Search This Blog
Saturday, April 25, 2020
Huu hapa ujumbe wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutoka kwa Rais Uturuki
Rais wa Uturuki na msemaji wa Bunge wawatakia waislamu wote funga na ibada njema za Mwezi Mtukufu wa Rmadhani.
Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan na msemaji wa bunge la taifa wawatakia waislamu wote ulimwenguni funga njema ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na ibada njema za mwezi huo mtukufu katika kalenda ya kiislamu.
Rais Erdoğan ameandika katika ukurasa wake wa Twitter ujumbe kuhusu kuingia kwa Mwezi Mtukufu wa Rmadhani na kuukaribisha kwa imani kama ilivyoagizwa na Mtume.
Katika ujumbe wake wa Twitter ulioambatanishwa na picha ya Al Kaaba na maneno yanayopatikana katika Quran Sura ya Pili Aya ya 183, aya ambayo inawakumbusha waislamu : "Enye waislamu, mmefaradhishiwa kufunga katika Mwezi Mtukufu wa Rmadhani kama walivyofaradhishiwa wakabla yenu ili muweze kuwa wachamungu".
Msemaji wa Bunge la Uturuki Mustafa Sentop nae pia amewatakia waislamu mwanzo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni kuwakumbusha kuendelea kuheshi maagizo yaliotolewa katika juhudi za kupambana na virusi vya corona na kujikinga na maambukizi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment