Search This Blog

Tuesday, April 7, 2020

Giroud ageuza kibao, anabaki zake Chelsea

LONDON, ENGLAND .OLIVIER Giroud ameripotiwa kubadili mawazo yake na kwamba yupo tayari kutulizana Chelsea baada ya kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya kwa ajili ya kubaki Stamford Bridge hadi msimu ujao.
Fowadi huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 33, mkataba wake wa sasa utafika tamati mwisho wa msimu huu na ilionekana kama vile The Blues watamfungulia mlango wa kutokea. Lakini, kwa taarifa zilizopatikana ni kwamba kumekuwa na mazungumzo ya kuhusu mkataba mpya.
Kwa sasa mambo hayatakamilika kabisa kutokana na watu wengi kuwa kujifungia vyumbani kutokana na kukwepa maambukizi ya virusi vya corona.
Lakini, kinachoelezwa kwamba pande hizo mbili zitafikia makubaliano ya kusaini dili jipya na Giroud ataendelea kuvaa jezi za Chelsea kwa msimu ujao.
Sera ya Chelsea ipo wazi ni kwamba inatoa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja tu kwa wachezaji wake waliozidi umri wa miaka 30.
Lakini, jambo hilo linaweza kubadilika kwa Giroud na kupewa miaka michache ya kukipiga kwenye kikosi hicho. Girouad, ambaye alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichobeba ubingwa wa Kombe la Dunia 2018, alitarajia kuachana na Chelsea kwenye dirisha la Januari. Tottenham Hotspur ya Jose Mourinho na Inter Milan ya Antonio Conte, ambao wote ni makocha wa zamani wa Chelsea walionekana kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...