
WAKALI wa muziki wa kizazi kipya walio wachumba kwa sasa, Nandy na Billnas wametakiwa kuendeleza walipofikia hivi sasa katika hatua inayofuata na sio kukaa muda mrefu wakati hatua nzuri wameifikia hivi sasa.
Wawili hao walivalishana pete ya uchumba ambayo ilikuwa siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Billnas ikiwa ni ishara ya kuja kuwa mke na mume baadaye, jambo lililoungwa mkono na G-Nako kutoka Kundi la Weusi aliyewataka sasa wafanye kweli kwa kufunga ndoa mapema.
G Nako amemtaka Bilinas kufuata hatua inayofuatia na sio kumvalisha pete miaka tisa binti wa watu bila hatua yoyote kufuatia.
“Baada ya pete mkubwa fanya umalize kabisa, sio tena miaka tisa tena ya kujuana hongera sana Billinas,” amesema mkali huyo anayetamba na ngoma yake ya Joto.
Naye mchekeshaji maarufu nchini, Jotti amewapongeza wawili hao kwa hatua waliyofikia na kuwataka wakamilishe inayofuata.
“Nawakaribisha kwenye chama, hongereni sana wadogo zangu kwa hatua nzuri ambayo mmeianza Mungu akawasimamie vyema kwenye ndoa yenu,” amesema Joti aliyejipatia umaarufu ndani ya Kaole Sanaa kabla ya kujiunga na kundi la Ze Commedy Show na baadaye Original Komedi akiwa na wakali wenzake, Masanja Mkandamizaji, MacReggan, Mpoki na Wakuvanga.
No comments:
Post a Comment