Search This Blog

Tuesday, April 7, 2020

FIFA kumaliza mzizi wa fitna kuhusu Corona

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) huenda likatoa taarifa ya kusimama kwa msimu wa 2019/20 kwa muda usiojulikana na kuzipa mamlaka vyama na mashirikisho ya nchi husika kuamua lini wataanza kucheza tena ligi zao.

Taarifa zinasema kuwa FIFA inatazamia kubadilisha tarehe ya dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi huku pia ikitaka kuwapa wachezaji ruhusa ya kuendelea kuzitumikia timu zao zaidi ya Juni, 30, kwa wale ambao mikataba yao itakuwa inamalizika katika tarehe hiyo.

Ripoti hiyo ambayo huenda ikatolewa kwenye siku mbili zijazo, itasaidia klabu za Ligi Kuu England, kuepukana na janga la kulipa kiasi kikubwa cha fedha kwa kampuni zilizonunua haki za matangazo ya runinga ambapo ikiwa msimu utamalizika bila ya mechi zilizosaliwa kuchezwa klabu zitatakiwa kutoa kiasi cha Pauni 726 milioni kulipa kampuni hizo.

Pia katika ripoti iliyotoka baada ya kikao kilichokaliwa na wawakilishi wa klabu na Shirkisho la Soka England hakukuwa na makubaliano juu ya lini hasa ligi hiyo itarejea, hivyo kulikuwa na sintofahamu ambayo FIFA wanaonekana kutaka kuiondoa kupitia ripoti hiyo wanayotaka kuiachia.

Katika ripoti hiyo watakuwa wamewapa ahueni nchi mbalimbali kuamua lini waanze kucheza ligi zao kulingana na hali ya maambukizi ya virusi hivyo itakavyokuwa kwenye nchi hizo.

Pia kwenye kikao hicho klabu zilitoa taarifa ya kuwa zitajaribu kuzungumza na wachezaji wao ili kuangalia uwezekano wa kupunguza mishahara yao kwa asilimia 30.

Kwa sasa baadhi ya klabu za Ligi Kuu England zinaamini kuwa mechi zilizobakia kwa msimu huu zinapaswa kuchezwa bila mashabiki  ili msimu umalizike kabla hata hali ya wasiwasi kuhusu maambukizi ya virusi hivyo haijaondoka.
Lakini klabu nyingine zina mawazo tofauti kabisa na zinaamini kuwa Ligi Kuu inapaswa kurudi wakati hali ikiwa shwari ili mashabiki nao wahudhurie viwanjani.

FIFA inaamini kuwa maambukizi ya virusi vya corona yana tofautiana kulingana na nchi husika hivyo ikiwa na maana kila nchi itakuwa na muda wake wenyewe wa kuruhusu mpira uchezwe pale hali watakapoona imekaa sawa.
 
FIFA pia inataka kutoa taarifa yakuwa mikataba ya wachezaji iweze kuwa endelevu ili wachezaji ambao mikataba yao itakuwa inaisha kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi waweze kumaliza msimu licha ya mikataba yao halisi kuwa imemalizika.

Hata hivyo hili limeonekana kuwa litaleta mkanganyiko kwa baadhi ya klabu England ambazo zinaona zitakuwa zinawalipa wachezaji mishahara ya bure bila ya wao kuingiza kitu chochote kwakuwa mechi hazitakuwa zinachezwa.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...