Search This Blog
Wednesday, April 29, 2020
Bei elekezi ya Sukari Yawaponza Wafanyabiashara Saba Wilayani Hai
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Sabaya ameyafunga maduka saba wilayani kwake huku wamiliki wakiwekwa chini ya ulinzi kwa kukiuka tangazo la Serikali kuhusu bei elekezi ya kuuza sukari.
Sabaya ametoa uamzi huo baada ya kufanya ziara ya kishtukiza leo Aprili 28, 2020 kwenye maduka hayo yaliyopo maeneo ya stendi kuu na kukuta sukari ikiuzwa kwa bei tofauti na iliyoelekezwa na Serikali hivi karibuni.
Aidha ametoa onyo kwa wafanyabishara wajumla katika wilaya hiyo kuuza sukari bei ambayo wafanyabisahara wadogo watauza kwa bei elekezi.
Waliofungiwa maduka yao walikuwa wakiuza bidhaa hiyo kwa bei ya Sh3, 500 badala ya 2,700 iliyoelekezwa na Serikali mkoani humo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment