
NEWCSTLE, ENGLAND . LISEMWALO ni kwamba Newcastle United watambeba kocha Massimiliano Allegri kuja kufanya kazi kma klabu hiyo itakuwa chini ya utawala mpya.
Kampuni ya Saudi Arabia iliyoongozwa na Mwana Mfalme, Mohammad Bin Salman imeripotiwa kuwa kwenye hatu za mwisho za mchakato wa kuinunua klabu hiyo kwa dau la Pauni 340 milioni kuitoa Newcastle kwenye mikono ya Mike Ashley, ambaye aliiweka sokoni klabu hiyo tangu Oktoba 2017.
Mwaandishi wa habari wa Italia, Fabio Santini, alisema kwamba wamiliki wapy wa Newcastle wamepanga kumchukua kocha wa zamani wa AC Milan na Juventus, Allegri kwenda kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo watakapoichukua timu rasmi. Timu hiyo kwa sasa inanolewa na Steve Bruce.
Allegri amekuwa hana kazi tangu alipoachana na Juventus mwaka jana, mahali ambapo alishinda mataji matano ya Serie A na manne ya Coppas Italia.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 aliahi kuhusishwa pia na klabu za Manchester United, lakini kuhusu mpango wa kwend Newcastle ameshamtambua kabisa kwamba straika anayecheza kwa mkopo Paris Saint-Germain, Mauro Icardi unweza kuwa usajili wake wa kwanza St James' Park.
Newcastle United kwa sasa inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, pointi nane juu ya timu juu ya shimo la kushuka daraja.
No comments:
Post a Comment