Search This Blog

Monday, March 16, 2020

Waziri Kairuki atoa misaada kwenye vituo vya watoto yatima na walemavu Same


Na Ferdinand Shayo,Same.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji ,Angellah  Kairuki atoa misaada katika vituo vya kulelea watoto yatima pamoja cha Rafiki Children Center na kituo cha watoto wenye ulemavu Wilayani Same cha Mama Kevin ikiwa ni njia mojawapo ya kuiwezesha jamii hiyo ambayo imekua ikisahaulika.

Kairuki amekabidhi vifaa mbalimbali kwa watoto  pamoja  pampers na sabuni pamoja na vyakula katika vituo vya Mama Kevin  pamoja na  Tumaini children center ambayo ni makao ya watoto.

Aidha amewapongeza walezi wa vituo hivyo kwa kazi kubwa wanaoyifanya ya kulea watoto katika misingi ya maadili mema ,uzalendo na kukua vizuri kiroho ii waweze kuwa na mchango katika jamii licha ya changamoto walizonazo sasa.

Amewataka wakazi wa same kuungana na kujenga utamaduni wa kusaidia watoto yatima walioko katika vituo ili waweze kukua vyema na kulijenga taifa lao.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...