Search This Blog

Sunday, March 1, 2020

Watumishi 92 wapewa mafunzo kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi



Na Adelina Ernes t Katavi.

Baadhi ya watumishi wa afya  wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamepata mafunzo dhidi ya kupambana na vifo vitokanavyo na uzazi hususani kifafa cha mimba na tatizo la kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua.

Akitoa takwimu ya vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Mganga mkuu Mkoa wa Katavi Dkt Omari Sukari amesema kwa mwaka 2018 wajawazito waliojifungua katika vituo vya afya  walikua 37,011 na waliopoteza maisha ni  53 na mwaka 2019 walikua 33,871 na miongoni mwao 48 waliopoteza maisha kwa tatizo la uzazi sanjari na kukosekana kwa gari la kubeba wagonjwa maarufu kama (Ambulance)

watoto wachanga waliopoteza maisha kwa mwaka 2018 walikua 581na 2019 wakiwa 499 sababu kubwa ikiwa ni  kutokuopo kwa chumba maalum cha kuhifadhia watoto kwa baadhi ya vituo vya afya.

"Tutapunguza vifo  vya mama na mtoto endapo kila mmoja wetu kuanzia ngazi ya Familia, jamii, kijiji, tasisi za kidini, serikali na wadau wa maendeleo tutashirikiana kutoa Elimu ya lishe bora kwa mama mjamzito"

Fuljensia Alex ni miongoni mwa wadau wa maendele hivyo ameomba uongozi wa mkoa wakishirikiana na wataalam wa Afya  kuhakikisha elimu  inawafikia watumishi wa vijijini kwani ndio waathirika zaidi wa tatizo hili kutokana na miundombinu isiyo rafiki.

Meneja wa chama cha wakunga Tanzania(TAMA) Lucy Mabada  amesema lengo la kutoa mafunzo hayo imeonekana vifo vingi  vinasababishwa na magonjwa ya kifafa cha mimba na kutoka damu nyingi wakati wakujifungua.

Licha ya sababu mbalimbali zinazopelekea vifo hivyo imegundulika kuwa asilimia 40 ya wanaopoteza maisha inatokana na lishe duni  na mkoa wa Katavi ni  miongoni mwa mikoa imeyoathirika na tatizo la utapiamlo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...