Search This Blog

Sunday, March 8, 2020

WANAWAKE WAMETAKIWA KUPAMBANA NA MAJANGILI WA WANYAMA PORI




Watumishi wa mamlaka ya Wanyamapori TAWA  Mkoa wa Morogoro wakiwa katika maanadamano,katika siku ya Wanawake Duniani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Watumishi wa mamlaka ya Wanyamapori TAWA  Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakiadhimisha  siku ya wanawake duniani katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

………………………………………………………………
NA FARIDA SAIDY MOROGORO.

Wakati dunia inaadhimisha siku ya mwanawake duniani wanawake nchini  wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya majangili ili kulinda nyala za serikali hususani wanyama pori.

Wito huo umetolewa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani,Manispaa ya Morogoro  na Bi Cassia Mayombo kutoka kitengo cha utawala mamlaka ya wanyama Pori (TAWA ) alikupokuwa anaongea na Fullshangwe Blog,ambapo amesema kuwa wao kama TAWA wanatambua mchango wa mwanamke katika kupambana na majangili.

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi Mwandamizi Mahusiano kwa Umma mamlaka ya Wanyama Pori (TAWA) Bwana Twah Twahibu amesema kuwa askari  wanawake wa wanyamapori(JESHI USU) wapo vizuri katika kupambana na majangili wawapo porini hivyo amewataka kuongeza kasi zaidi katika kazi yao.

Aidha amesema kuwa mamlaka hiyo ipo katika mchakato wa kufungua mabucha na mashamba ya kufugia wanyamapori,hivyo wamewataka wadau mbalimbali kujitokeza kuomba nafasi hizo zitakazokuza kipato chao na taifa kwa ujumla.. 

Katika hatua nyingine amewataka wananchi hususani wa mkoa wa morogoro kutumia njia mbadala ya kuwafukuza tembo wanaoingia katika mashamba yao kwakuweka mizinga ya nyuki jambo litakalowasaidia kuepukana na wanyama hao kipindi mamlaka ikiwa inaagalia namna ya kukabiliana na wanyama hao.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...