
MADRID, HISPANIA . STAA wa Real Madrid, Vinicius Junior amefunguka sababu za beki wa kati wa Barcelona, Gerard Pique kumuita chizi wakati wa pambano la El Clasico ambalo lilizikutanisha timu hizo kubwa Hispania na Madridi kushinda 2-0.
Wawili hao walionekana kutupiana maneno baada ya Vinicius kudai kuwa alifanyiwa faulo kwenye eneo la hatari lakini mwamuzi hakupiga filimbi kuashiria ilikuwa penalty.
Vinicius alisema “Pique aliniambia ‘sikukugusa, sikukugusa’, lakini nilidhani kuwa alinichezea madhambi, lakini nilipoangalia picha za video kwenye YouTube niligundua kuwa ni Arthur, ndiye alinifanyia madhambi”
Kinda huyo anadai kuwa hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya Pique kumuita chizi, kwa sababu alimshangaa kwa nini anamsingizia kuwa kamfanyia faulo wakati kiuhalisia ni mchezaji mwingine ndiye aliyemkwaa.
No comments:
Post a Comment